Jumanne 19 Agosti 2025 - 15:48
Ikiwa kutatokea mgongano kati ya mume/mke na wazazi, tumchague yupi?

Hawzah/ Kuanza maisha ya ndoa haina maana ya kuiacha familia; bali kunahitaji kuwepo mipaka salama, ambapo heshima ya wazazi inalindwa na utulivu wa maisha ya ndoa unadumishwa

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam Yusufzadeh, mmoja wa wataalamu wa tiba ya wanandoa na tiba ya kifamilia, katika makala yake aligusia suala la kuingiliwa kwa familia, na akaandika:

Familia ni mizizi na nguzo yetu, na wazazi ndio neema tukufu zaidi katika maisha. Lakini tangia pale unapooa au kuolewa, mwenzi wako ndiye anayekuwa mshirika mkuu wa safari ya maisha yako ya baadaye.

Ni jambo la kawaida kwamba katika baadhi ya mazingira kunatokea tofauti ya kimtazamo au sintofahamu kati ya wanandoa na wazazi.

Kanuni kuu ni kuyasimamia kwa busara mahusiano haya; si kuchagua upande mmoja na kuuacha mwingine!

Kanuni ya kwanza na muhimu zaidi ni kuilinda heshima na kumheshimu baba na mama, kamwe tusiruhusu maneno au vitendo vyetu kudhoofisha hadhi na nafasi ya wazazi.

Hata hivyo, kuingia katika maisha ya ndoa kunahitajia kuwepo mipaka ya wazi na yenye heshima kati ya wazazi na wanandoa.

Kwa hakika, “kuweka mipaka yenye salama” kutasaidia heshima ya wazazi ibakie salama, na wakati huo huo utulivu wa maisha ya ndoa udumu.

Ikiwa mahusiano ya kifamilia hayatakuwa na usimamizi na mipaka, kwa kutaka au bila kutaka, kutazuka mivutano na ukosefu wa heshima; na madhara yake yatawafikia wanandoa na pia wazazi.

Kitendo cha Uislamu kusisitiza juu ya kuilinda heshima ya wazazi, maana yake ni: usifanye jambo litakalovunja heshima ya baba na mama!

Ukosefu wa usimamizi wa mahusiano ya kifamilia ndio chanzo cha dharau na ukosefu wa heshima…

Suluhisho:
Linda uhusiano wako wa ndoa kwa mapenzi lakini pia ukiwa na msimamo thabiti.

Matatizo binafsi yanayo patikana katika maisha ya ndoa yasielezwe kwenye familia.

Ikiwa kutatokea tofauti kubwa, tafuteni msaada kutoka kwa wasuluhishi waaminifu au mshauri mtaalamu.


Kumbuka: kumpa kipaumbele mwenza wako haina maana ya kutokuipenda familia; bali ni kuchagua ukomavu, heshima na utulivu kwa kila mwanafamilia.

Mabadiliko yanaanza kutoka kwako.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha